Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa kinatafakari ushauri uliotolewa na wazee wa chama hicho kuhusu kumpa nafasi Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais – Zanzibar.

Tamko hilo la Chadema ambalo limetolewa leo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji limekuja kufuatia kauli ya wazee waliodai kuwa kama CUF itaendelea kuwa na mpasuko Zanzibar, wao watamualika Maalim Seif agombee urais wa Zanzibar.

Dkt Vicent Mashinji, Katibu Mkuu – Chadema

“Wale ni wazee walitoa maoni yao, hivyo chama kitajadili na kutoa tamko,” Dkt. Mashinji anakaririwa akiwa Dar es Salaam.

Wazee wa Chadema kupitia kwa mwenyekiti wao, Hashimu Juma, wakiongea na waandishi wa habari wiki hii walisema kuwa nafasi hiyo atakayopewa Maalim Seif wataomba na wabunge wake wapewe pia na kumpa nafasi ileile ndani ya chama, kwakuwa lengo ni kuwaleta maendeleo.

Diamond, Lil Wayne uso kwa uso ndani ya kolabo moja
Muna amkana anayedaiwa kuwa mwanaye

Comments

comments