Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo John Mnyika, ameiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuitaarifu kutoshiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Ngorongoro huku ikiwaonya watakaochukua fomu kwa jina la chama hicho.

Mnyika amesema msimamo wa chama hicho bado ni kutoshiriki uchaguzi hadi kufanyika mabadiliko ya tume ya uchaguzi ambapo wanataka iundwe Tume Huru itakayohakikisha Chaguzi zinakua na Haki na Halali.

Hapo jana Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi ilitangaza jina la Mgombea wa Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo hilo ambaye ni Ndugu Emmanuel Lekishon Shangai.

Uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, William Ole Nasha aliyefariki Septemba 27 jijini Dodoma na unatarajiwa kufanyika tarehe 11 Disemba 2021.

Pablo Franco awakubali mashabiki SImba SC
Musiba kukata Rufaa dhidi ya hukumu ya Bilioni 6.