Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kinatarajia kutoa hatma ya wabunge wake wawili, Saed Kubenea wa jimbo la Ubungo pamoja na Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini, Antony Komu kufuatia wabunge hao kudaiwa kupanga njama za kumdhuru moja ya mwanachama mwenzao.

Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kuwa hatma ya wabunge hao inatarajia kujulikana kufuatia kikao cha dharura cha wajumbe wa kamati kuu wa chama hicho walioketi wakiongozwa na Mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Mbowe.

“Kamati kuu imeitishwa na tukawaita wabunge hao wawili, tumeshamaliza kumhoji mheshimiwa, Antony Komu na sasa tunaendelea na mahojiano na mheshimiwa Kubenea, Kwa kuzingatia  mamlaka ya nidhamu ya kamati kuu kwenye chama chetu, tutapata wasaa wa kuwaita waandishi wa habari ili kuzungumza na kwa mwenendo unavyokwenda maamuzi hayo yatatolewa, ameongeza John Mrema

Aidha, hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, ilisambaa sauti fupi ikimuhusisha mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea pamoja na Mbunge wa Moshi Vijijini, Antony Komu ikisikika wabunge hao wakipanga njama ya kumzuru Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob.

 

 

Video: Musiba amvaa Lema, adai ni njama za Chadema
Unatafuta ajira? haya hapa makampuni 10 yanakutangazia wewe nafasi za ajira

Comments

comments