Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimebeza juhudi za utumbuaji majipu na sera ya ‘Hapa Kazi Tu’ inayoongozwa na Rais John Magufuli na kuulinganisha na utawala wa serikali iliyopita.

Dk. Vicent

Dk. Vicent Mashinji

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji amesema kuwa sera ya ‘Hapa Kazi Tu’ na operesheni ya utumbuaji majipu umekosa dira.

“Kuna vitu vingi vinafanyika lakini hatujui kipi ni kipi na wapi tunaelekea. Kuna mambo mengi yananyika, lakini hakuna mtu mmoja kwenye nchi hii anajua lina mpango gani na linaelekea wapi,” Dk. Mashiji anakaririwa na gazeti la Mwananchi.

Dk. Mashiji ameulinganisha utawala Serikali iliyoko madarakani na ile ya awamu ya nne iliyoongozwa na Dk. Jakaya Kikwete, ambapo amedai sera ya utawala uliopita wa ‘Maisha Bora kwa Kila Mtanzania’ ilikuwa bora zaidi kwani ilionesha muelekeo.

“Rais Kikwete alituambia maisha bora kwa kila Mtanzania, na tulijua maisha hayo yanapatikana kwa kila mmoja kupambana wenyewe na tulipambana. Lakini sasa hatujui tunaelekea wapi, alisema Dk. Mashinji.

“Hapa Kazi tu! Umemfukuza huyu kazi halafu nini kitaendelea? Keshaondoka kakuacha, utaajiri mtu mwingine? Tunahitaji mtu wa kujibu hayo maswali. Nchi yote sasa inavurugwa,” aliongeza.

Viongozi wa Chadema wamekuwa wakipinga utaratibu wa utumbuaji majipu unaofanyika wakidai kuwa kwa kiasi kikubwa haufuati utaratibu na sheria za nchi.

Mpinzani wa Museveni ajiapisha kuwa Rais, Kilichomkuta…
Tanzia: Mchekeshaji maarufu wa 'Vituko Show' afariki