Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) kimedai kuwa kinawakusanya wafuasi wake mjini Dodoma kwa lengo la kusaidia kuzuia mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliolenga kumkabidhi Rais John Magufuli, uenyekiti wa chama hicho, Julai 23 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi, zimeeleza kuwa chama hicho kimepanga kuwakusanya wafuasi wake kwa madai kuwa watalisaidia Jeshi la Polisi kuzuia mkutano huo kwakuwa tayari Polisi walitoa agizo la kutofanyika kwa mikutano yote ya kisiasa nchini.

“Kwahiyo katika kutekeleza agizo hilo la Polisi tarehe 23 tutakusanyika kwa wingi Dodoma kuzuia mkutano huo haramu na kuisaidia CCM kutii sheria bila shuruti,” alisema  Sosopi katika taarifa yake.

Hivi karibuni kulikuwa na vutankuvute kati ya Polisi na vyama vya upinzani kuhusu kufanyika au kutofanyika kwa mikutano ya kisiasa ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kutoa tamko rasmi kuzuia mikutano yote ya kisiasa wakitoa sababu za kiusalama.

Tanzia: Aliyekuwa Mbunge wa Kilindi, Shellukindo afariki
Video: Thurman Vs Porter lavunja rekodi ya ndondi, wamfuata Muhammad Ali