Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelalamikia utaratibu mzima wa upigaji kura katika jimbo la Ukonga lililopo jijini Dar es salaam.

Malalamiko hayo yametolewa na Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika alipokuwa akizungumza wa waandishi wa habari jijini Dar es salaaam, ambapo amesema kuwa mawakala wengi wa Chadema wamekamatwa na kupelekwa katika kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo jijini humo.

Amesema kuwa kama chama wamefanya mawasiliano na Tume ya Uchaguzi lakini hakuna ushirikiano uliotolewa kuhusu hujuma hizo.

“Tumewasiliana na tume lakini tume mpaka sasa haijatupa ushirikiano wowote, kitu ambacho kinaashilia kuwa hujuma hizi wamezipanga kwa kusema watashughulikia tatizo hili,” amesema Mnyika

Video: Mgombea ajiuzulu DAKIKA 1 KABLA YA KURA KUPIGWA | Ammwagia sifa mpinzani wake hadharani

Chadema: Mawakala wetu wananyanyaswa kwenye vituo vya kupigia kura
Mstari wa Eminem kuhusu Diddy kusababisha kifo cha Tupac 'ni shida'

Comments

comments