Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa sababu za kutohudhuria katika uzinduzi wa barabara ya juu ‘Flyover’ katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam.

Wabunge wa upinzani kupitia Chadema jijini Dar es salaam ni John Mnyika wa jimbo la Kibamba, Halima Mdee wa jimbo la Kawe pamoja na Saed Kubenea wa jimbo la Ubungo, ambapo wote hawakuhudhuria katika uzinduzi huo.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, amesema kuwa sababu zilizowafanya Wabunge wa Kawe, Halima Mdee na wa Kibamba, John Mnyika kutokufika katika uzinduzi huo walikuwa na kesi katika Mahakama ya Kisutu.

“Tumemsikia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisema, Wabunge wa CHADEMA, walialikwa kwenye uzinduzi huo na hawakufika, walikuwa Mahakamani wakati shughuli zikiendelea, hivyo wasingeweza kuwa Mahakamani na wakati huohuo wakahudhuria uzinduzi,”amesema Mrema.

Hata hivyo, ameongeza kuwa yeye kama kiongozi anajua taratibu za kuwasiliana na viongozi kwa kupokea mwaliko rasmi, lakini si kupokea mwaliko wa viongozi kupitia vyombo vya habari, bali inatakiwa kufuata utaratibu wa kiserikali.

 

TANESCO yawaomba radhi wateja wake
Breaking News: Mbunge Marwa ajiuzulu Chadema na kutimkia CCM