Chama Cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshtaki Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kwenye Shirikisho la Soka Duniani FIFA kutokana na kauli za kibaguzi alizozitoa hivi karibuni.

Chama hicho kimesema kuwa kimemwandikia barua Rais wa FIFA na nakala nyingine ikipitia kwa Shirikisho la Soka Afrika CAF pamoja na ushahidi wa video inayomuonyesha akizungumza kauli hiyo.

“Tunaandika barua hii kuelezea masikitiko yetu na kupinga kauli iliyotolewa na Rais wa TFF, Wallace Karia ambayo inaunga mkono uvunjaji wa haki za binadamu, uhuru wa kuzungumza na kuchochea ubaguzi wa kisiasa jambo ambalo ni kinyume na miiko ya mchezo wa mpira wa miguu unaosimamiwa na FIFA,” imeeleza sehemu ya barua hiyo ambayo imesainiwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene.

Aidha, katika mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika Februari 2 Jijini Arusha, Karia alikemea watu wenye tabia alizoziita za ‘U-Tundu Lissu’ katika soka, kuwa kamwe hawezi kukubali kuona wakiendelea kukosoa uongozi wa TFF.

Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa TFF, Wallace Karia pia aliwaomba msamaha wafuasi wa Chadema kama kuna watu ambao aliwakwaza kutokana na kauli hiyo.

 

Mollel adai Kushambuliwa Lissu kwa risasi ni mpango wa Chadema
Mfumuko wa bei wa taifa waendelea kushuka hadi asilimia 3.0