Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza uamuzi wa kumvua uanachama aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Songea Mjini, Joseph Fuime kwa tuhuma za kukihujumu chama hicho.

Joseph Fuime

Joseph Fuime

Akitoa ufafanuzi kuhusu uamuzi huo, Katibu wa Chadema Wilaya Songea Mjini, Olais Ng’ohison amesema kuwa uamuzi huo ulifikiwa Oktoba 23 mwaka huu baada ya kujiridhisha kuwa Fuime alihujumu matokeo ya uchaguzi akiwa mgombea.

Ng’ohison alisema kuwa pamoja na mambo mengine, Fuime hakushirikia katika zoezi la ujumuishaji wa matokeo huku akiwa amezima simu zake zote huku akijua anatafutwa.

Fuime anatuhumiwa kuuza nafasi ya ushindi wa chama hicho kwa njia ya hujuma hizo.

Wahitimu vyuo vikuu watakiwa kuchangamkia fursa za ajira
Video: Kauli ya Samuel Sitta yamtoa machozi Majaliwa, Nape naye...