Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeamua kuingilia kati kufuatia kauli ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kusema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu lissu anaweza kuondolewa Ubunge wake kufuatia kiongozi huyo kufanya ziara nchini Uingereza bila kibali cha Spika.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema ambapo amesema kuwa kauli ya Spika haina tija kwa kuwa Tundu Lissu bado hajapewa ruhusa na Daktari wake kurejea nchini kwa madai kuwa amepona kabisa.

“Spika si Daktari mpaka aseme kuwa Lissu amepona na hajawahi kumtembelea kwa kipindi chote tokea apelekwe hospitali. Tunakumbuka aliyewahi kuwa waziri wakati wa serikali ya awamu ya nne, Prof. Mwandosya aliugua kwa zaidi ya mwaka, lakini hatukusikia kauli za aina hii.”

Aidha, akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari, Spika Ndugai alimtaka Mbunge Tundu Lissu huyo kurejea nchini ili kuendelea na shughuli za Bunge kwa kuwa hana kibali cha kuwa nje ya nchi.

Hata hivyo, Spika Ndugai aliongeza kuwa Lissu hana ruhusa ya kuwa nje ya Bunge, hivyo anatakiwa kurejea nchini kuendelea na shughuli za ubunge kama ilivyo kawaida ya wabunge.

 

Video: Ufugaji mende unavyolipa
Mnangagwa maji ya shingo, asitisha ziara yake ya nchi za Nje

Comments

comments