Chama cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA) kimekanusha habari inayoenea kuhusu Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kujivua uanachama na kuhamia CCM, na kusema kuwa tetesi hizo hazina ukweli wowote na zinapaswa kupuuzwa.

Chadema imekanusha fununu hizo kupitia mtandao wake wa Twittter kwenye ukurasa wa chama hicho na kusema kwamba wanaosambaza habari za Mnyika kujivua ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya maisha ya watanzania.

 “Kuna taarifa zinasambazwa mitandaoni ya kuwa Mhe. John Mnyika, Mbunge wa Kibamba amejivua uanachama wa CHADEMA. Taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote, ni za kupuuzwa, wanaozisambaza ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya hali ya maisha ya Watanzania.

Video: Nyuma ya pazia shambulio la Lissu, Mtoto wa kike wa miaka 7 abainika wa kiume
McMaster atahadharisha kutokea kwa vita kali