Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ametoa tangazo la fungua milango kwa mwanachama yeyote anayetaka kugombea nafasi ya Urais kupitia chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jiini Dar es salaam, leo Juni 3, amesema kuwa, fomu kwa ajili ya wagombea wa kiti cha Urais zitaanza kutolewa hii leo hadi June 15 mwaka huu.

Kuhusu watu waliojitokeza kutangaza nia ya kiti cha urais kupitia chama hicho kwa vyombo vya habari amesema hawezi kuwazungumzia kwani mpaka sasa hivi bado hawajawasilisha barua zao ndani ya ofisi yake.

“Utaratibu unaohusika na mchakato huu ni kuandika barua kwa Katibu Mkuu, tukishapata barua rasmi Kamati Kuu itakaa na kuwatafakari na kutoa mweleke, na wale ambao wametia nia kwenye vyombo vya habari na barua zao hazijafika kwa katibu Mkuu wa chama siwezi kuwazungumzia”¬†amesema Mnyika.

Ameongeza kuwa CHADEMA pia imefungua milango kwa vyama vyote vya siasa nchini ili kufanya majadiliano na vyama hivyo yenye lengo la kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.

Tshabalala awatoa hofu mashabiki Simba SC
Vyuo vyapewa siku 3 kukamilisha mgao fedha za kujikimu kwa wanafunzi