Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, Tundu Lissu amefafanua kwamba chama chake hakijafungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya The Hague (ICC), kwa sababu haina mamlaka ya kisheria ya kufanya hivyo.

Amesema nchi wanachama ambao wametia saini mkataba wa Roma na mwendesha mashtaka mkuu wa ICC ndiyo pekee walio na mamlaka ya kisheria kufungua kesi katika Mahakama hiyo yenye makazi yake nchini Uholanzi.

Lissu ambaye alikuwa akizungumza wakati wa mjadala mtandaoni, alisema mchakato huo unaweza kukabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao wana nguvu ya kura ya Veto.

Lissu amesema Chadema imewasilisha ushahidi juu ya matukio ambayo yanakidhi vigezo vya kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu ambao umefanywa ukilenga wanachama wa upinzani.

Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Prof Adelardus Kilangi hivi karibuni alisema hakuwa anafahamu kama Chadema ilikuwa imeishitaki serikali katika Mahakama ya ICC kama alivyoeleza mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari kuanza kutumika Januari 2022.

Lissu amesema ICC ambayo ilianzishwa mwaka 1999 inashughulika na aina nne za kesi ikiwa ni pamoja na zile zinazohusiana na mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu wa kivita na uchokozi baina ya mataifa.

“Ni jukumu la mwendesha mashtaka kuangalia kama ushahidi wetu unaendana na Kifungu cha 7 na 17 cha mkataba wa Roma ambao unabainisha aina za makosa ya uhalifu na kama yana uzito wa kutosha,” amesema Lissu.

Maombolezo ya siku tatu kufuatia vifo vya mawaziri wawili
Ufungaji bora wamnyemelea Miraji Athuman