Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mrema amesema kuwa taarifa zinazozagaa kuwa chama hicho kimesusia uchaguzi hazina ukweli wowote na kudai wanaofanya hivyo ni kundi la watu wachache wenye lengo la kutaka kupotosha umma ili kesho wasiende kupigia kura.
 
Aidha, taarifa zilizosambaa mitandaoni zimesema kuwa chama hicho kimejitoa katika uchaguzi mdogo wa marudio kwenye jimbo la Kinondoni, Siha na kata nane nchini.
 
“Taarifa hizo ni za uongo zinasambazwa na watu ambao wameshashindwa naomba watu wazipuuze, tunapozungumza sasa hivi Mwenyekiti wa chama Mhe. Mbowe anahitimisha kampeni katika jimbo la Kinondoni na Mhe. Lowassa yupo kule Siha nae anahitimisha kampeni,”amesema Mrema. 
 
Hata hivyo, Mrema amezidi kuwasisitizia wananchi kuzipuuza taarifa zozote zinazotoka kuhusu kutoshiriki uchaguzi huku akiwaomba wananchi katika Jimbo la Kinondoni na Siha kujitokeza kwa wingi kesho kushiriki kupiga kura kwa sababu ni haki yao ya msingi.
 
  • Video: Acheni propaganda za nani hapigi kura- Salum Mwalimu
  • Video: Lowassa amenifundisha mengi- Bashe
  • Video: Bashe adai hamjui Rais Dkt. Magufuli

Dkt. Nchemba: Demokrasia si kukatana mapanga
Video: Dkt. Slaa afunguka mazito baada ya kuapishwa