Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kupeleka mashtaka yake katika Kamati ya Maadili kumshataki Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu ambaye alishiriki kufanya kampeni kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Siha.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, ambapo amesema watafikisha mashtaka yao kwenye Tume ya Maadili kama ambavyo wameshauriwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).

“Tunapeleka mashtaka leo kwenye kamati ya maadili, tulipanga kupeleka saa tano asubuhi kwa hiyo mashtaka yatakwenda muda huu kumshtaki rasmi Mkuu wa Wilaya,”amesema Mrema

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu alipanda jukwaani kumnadi mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Siha, Dkt. Godwin Mollel, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Hata hivyo, Wakuu wa Wilaya, Mikoa na Wakurugenzi hawapaswi kushiriki katika masuala ya siasa, na hii imetokea ikiwa tayari Tume ya Uchaguzi ilishatoa onyo kwa viongozi hao kutothubutu kushiriki katika masuala ya siasa

Karia atuma salamu za rambirambi msiba wa Ntambi, Ismail Suma
Kandege avunja mkataba wa TBA na Halmashauri