Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kampeni maalum ya kuchangia fedha kwaajili ya kugharamia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayetibiwa huko jijini Nairobi nchini Kenya huku matibabu hayo yakigharimu shilingi milioni 10 kwa siku.

Aidha, chama hicho kimeomba msaada kwa jumuiya za kimataifa ikiwemo Ujerumani na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) kusaidia kulipia gharama za matibabu ambazo zimekuwa ni kubwa kupita kiasi.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari, ambapo amesema kuwa pamoja na kuwa gharama za kumtibu Lissu kuwa ni kubwa lakini chama kitaendelea kumpigania.

“Unajua chama tumepoteza watu wengi sana, kama vile Ben Saanane, Dkt. Slaa, lakini tuna mahaba makubwa sana na ndugu yetu Lissu, hivyo tunaendelea kupigania maisha yake, gharama za matibabu ni kubwa mno, maana kwa siku anatumia gharama ya shilingi milioni 10, sasa sisi peke yetu hatuwezi, ndiyo maana tunaomba msaada kwa marafiki zetu,”amesema Prof. Safari

Hata hivyo, Prof. Safari amesema kuwa chama kimejaribu kukusanya fedha kutoka Kanda mbalimbali, na wananchi wamejitokeza kuchangia lakini kila siku gharama zinazidi kuongezeka hali ambayo imepelekea kupiga hodi katika Jumuiya za kimataifa.

 

TCRA yaja na mwarobaini kudhibiti wapotoshaji mtandaoni
Zuber Katwila atamba kurejesha enzi za 1999, 2000