Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelitaka jeshi la polisi nchini kutolea tamko kuhusu watu 40 waliokamatwa kwenye maandamano ya chama yaliyofanyika Februari 16, 2018 jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama hicho na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, ambapo amelitaka jeshi hilo kutoa kauli juu ya watu hao.

Amesema kuwa kama jeshi hilo likishindwa kuwapatia dhamana na kuwatolea ufafanuzi watu hao, basi ifikapo kesho wapelekwe mahakamani.

“Jeshi la Polisi mpaka hivi sasa wamekwisha vunja sheria kwa kutowapa dhamana wala kuwafikisha Mahakamani. Tunalitaka Jeshi la Polisi kupitia kwa IGP na Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, kutoa kauli leo juu ya hao ambao wanawashikilia na kuwanyima dhamana na kutowafikisha Mahakamani,”amesema Mnyika

Hata hivyo, Mnyika ameongeza kuwa taarifa walizokuwa nazo Jeshi la Polisi liliwakamata watu wengine ambao walikuwa wanajishughulisha na shughuli zao huku wengine wakiwa wametoka kushuka kwenye daladala.

 

St Louis wakataa kufungwa kwao
Mkuu wa wilaya amshukuru mumewe kuongeza mke