Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imeteua wagombea wake wa ubunge katika majimbo matatu.

Aidha, walioteuliwa na majimbo watakayowania katika mabano ni Asia Msangi (Ukonga), Amina Saguti (Korogwe Vijijini) na Yonas Laiser (Monduli).

Hata hivyo, katika taarifa iliyotolewa leo na Chadema Agosti 17, 2018 na mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene imesema kuwa wagombea hao wamepitishwa katika kikao maalum cha kamati kuu kilichoketi kwa siku mbili kati ya juzi na jana.

“Kamati Kuu ya Chama imefanya uteuzi huo wa wagombea ubunge kwa mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya mwaka 2006, toleo la mwaka 2016, ibara ya 7.7.16(q),” amesema Makene

DC Murro atangaza vita dhidi ya wanaume waliotelekeza watoto
Nape ataka watungiwe sheria kali wanaohama vyama