Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewavua nyadhifa zote ndani ya chama hicho mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea pamoja na mbunge wa Moshi Vjijini, Anthony Komu kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, John Mnyika alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa wabunge hao wamevuliwa nyadhifa kwa kosa la utovu wa nidhamu baada ya kuvuja kwa mazunbumzo yao kwenye mitandao ya kijamii.

“Tumeamua kuwavua nyadhifa zote za uongozi ndani ya Chadema wabunge hawa na kuwaweka chini ya uangalizi kwa muda wa miezi kumi na mbili, yaani mwaka mmoja, haya yote tunayafanya kwa ajili ya uhai na afya ya chama chetu,”amesema Mnyika

Kwa upande wake mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu amesema kuwa chanzo cha kuvuja kwa mazungumzo hayo ni yeye hivyo amewaomba radhi viongozi na wanachama wa chama hicho.

Naye mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea amesema kuwa katika mazungumzo hayo, hapakuwa na nia yeyote ovu.

 

Prof. Mbarawa azindua kampeni ya upandaji miti
Video: Zitto aibua maswali tata utekwaji wa Mo Dewji, Maajabu 12 ya Fry-Over Tazara

Comments

comments