Kuelekea Uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wamekwenda makao makuu ya Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC kudai viapo vya mawakala wa chama hicho katika uchaguzi huo.

Baada ya kufika katika ofisi hizo leo, Mbowe na viongozi hao wameelekea moja kwa moja katika ofisi za Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima.

Mbowe amewaambia waandishi wa habari kuwa wamefika ofisini kwake hawajamkuta hivyo ikawabidi wapige simu yake ya mkononi, na baadaye kubainisha kuwa Mkurugenzi huyo amewataka waorodheshe madai yao na kumpa taarifa hiyo.

Ambapo Mbowe amesema Chadema ina malalamiko mbalimbali kwa NEC, ametaja malalamiko hayo ni pamoja na.

  1. Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni kukataa kuwaapisha mawakala wa ziada, kwamba vituo vipo 613 na ameapisha mawakala 613.
  2. Kailima kukataa wabunge na madiwani wa Chadema kuwa mawakala
  3. Kailima kuja na sharti jipya kutaka mawakala wote wawe na vitambulisho
  4. kutotolewa kwa hati za kiapo kwa mawakala hadi sasa
  5. kituo cha majumuisho ya kura hakijafahamika hadi sasa

”Tumekubaliana naye katika hilo na nimewaita wabunge tumeingia kwenye chumba maalumu hapa NEC ili kuorodhesha madai yetu” amesema Mbowe.

Hata hivyo Kailima amewaahidi kuwatafutia ufumbuzi wa madao yao leo.

.

Video: Ndomba amfunda Meja Jenerali Yakubu
Video: Ramaphosa aapishwa kuwa Rais wa Afrika Kusini