Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeukwepa mpango wa Serikali kuhamia mjini Dodoma kwa madai kuwa  sio sehemu ya ajenda yake.

Akizungumza  hivi karibuni jijini Dar es Salaam,  Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji alisema chama hicho hakina mpango huo kwa sababu hayo ni masuala ya kisiasa yasiyo na msingi kiuhalisia.

“Sisi makao yetu makuu yapo Dar es Salaam, hata katiba yetu ndivyo inavyosema, tutaendelea kuwa hapahapa, “alisema Dk. Mashinji.

“Hayo ni mambo ya kisiasa yasiyo na misingi ya kiuhalisia, hata mazingira hayaruhusu, kwa hiyo sisi tutaendelea kuwa hapa (Dar es Salaam),” aliongeza.

Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Serikali ya awamu ya Tano ikiendelea na muchakato wa kuhamishia makao makuu yake mjini Dodoma, ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitangaza kuhamia mjini humo mwezi Septemba mwaka huu.

Rais John Magufuli alitangaza kuwa kufikia mwaka 2020, atakuwa ametimiza mpango huo ulioasisiwa na Serikali ya awamu ya kwanza iliyokuwa unaongozwa na Mwalimu Julius Nyerere.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alikuwa Kiongozi wa kwanza wa Chadema kukosoa hadharani uamuzi huo wa kuhamia Dodoma akidai kuwa uamuzi huo unechukuliwa bila kufanya utafiti wa mahitaji na mazingira ya sasa.

“Huwezi kutumia tathmini na maamuzi ya miaka 50 iliyopita kutekeleza mpango wa sasa kwa njia ileile. Ilipaswa kufanya kwanza tathmini kwa mazingira ya sasa, ” Profesa Baregu anakaririwa.

Mesut Ozil Aitaka Jezi Namba 10 Atamani Kuwa Zinedine Zidane
Nay Wa Mitego Atokwa Na Povu, Ni Baada Ya Shamsa Ford Kuolewa, Amchimba Mkwara Mwanaume Aliyemuoa