Watu wawili wa familia moja, mke na mume wakazi wa Kijiji cha Baga, Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, juni 19, 2017 saa saba mchana  wamefariki dunia baada ya kunywa chai ya rangi inayodhaniwa kuwa na sumu.

Mbali na hilo, mpwa wao amenusurika katika tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo bwana Rajabu Ally mwenye umri wa miaka 73, na bibi Amina Rajabu mwenye umri wa miaka 62, walipoteza maisha wakiwa wanapata  matibabu katika zahanati ya Baga

Kamanda wa polisi amesema katika tukio hilo mpwa wao Adam Said mwenye umri wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la tatu amenusurika katika kifo hiko.

”Katika tukio hilo ambalo limepoteza watu wa familia moja, mpwa wao alinusurika baada ya kunywa chai idhaniwayo kuwa ni yenye sumu, hivyo uchunguzi wa kina unaendelea kufanyika kubaini kilichojiri na aliyesababisha” amesema Benedict Wakulyamba, kamanda wa polisi Tanga.

 

Ripoti: Jokofu chanzo cha kuteketea kwa moto jengo la London
Ukiukwaji wa kanuni katika uchaguzi wamchefua Kinana