Chama cha Ujerumani kinachopigia debe mazingira rafiki ya biashara cha FDP kiliidhinisha kwa wingi makubaliano ya serikali ya muungano yaliyofikiwa baina yake na chama cha Social Democrats SPD na kile cha kijani.

Katika mkutano maalumu wa FDP uliofanyika kwa njia ya vidio mjini Berlin, asilimia 92 ya wajumbe wa mkutano huo walipiga kura ya kuunga mkono makubaliano ya uundwaji wa serikali ya muungano.

Wajumbe wa SPD waliidhinisha kwa wingi makubaliano hayo siku ya Jumamosi.

Chama cha kijani bado kipo katika mchakato wa kupiga kura kwa ajili ya kupitisha makubaliano hayo.

Ikiwa vyama vyote vitatu vitakubaliana na mpango huo, makubaliano yatasainiwa rasmi na kumruhusu Olaf Scholz kutafuta kupitishwa rasmi katika bunge la Bundestag siku ya Jumatano na kuchukua mikoba ya Angela Merkel kama kansela.

Simba SC yatangaza viingilio Desemba 11
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Disemba 6, 2021