Chama cha upinzani cha Kisoshalisti SPD nchini Ujerumani, Jumapili hii kitaamua juu ya kuanza mazungumzo kuhusu kuunda muungano na Chama tawala cha Kihafidhina cha kansela Angela Merkel, hatua ambayo itasaidia kuisogeza mbele nchi hiyo katika kupata serikali imara.

Mwenyekiti wa Chama hicho, Martin Schulz anakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa makundi ya vijana ndani ya chama hicho hasa lile la msimamo mkali wa mrengo wa kushoto, ambayo yanahoji kuwa chama cha SPD kinapaswa kujijenga upya kikiwa upande wa upinzani.

Aidha, karibu wajumbe 600 wanatarajia kukutana mjini Bonn, kujadili na kupiga kura juu ya iwapo viongozi wao wanapaswa kuendelea na majadiliano ya kujiunga na Chama tawala cha Kihafidhina cha Merkel kilichoingia madarakani tangu mwaka 2013.

Aidha, pande hizo mbili, ambazo zote zilipoteza uungwaji mkono na chama cha siasa kali za mrengo mkali wa kulia cha AfD katika uchaguzi wa Septemba 24, zilifikia makubaliano ya awali wiki iliyopita lakini wakosoaji, akiwemo kiongozi wa tawi la vijana la chama cha SPD, Kevin Kuehnert, wamesema makubaliano yaliofikiwa hayajajumuisha masuala ya kutosha yanayosimamia SPD.

 

 

 

Marekani yasitisha baadhi ya huduma za kijamii
Magazeti ya Tanzania leo Januari 21, 2018