Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal Pappe Ousmane Sakho amekubali kubadilisha namba ya jezi aliyokua akiitumikia tangu mwanzoni mwa msimu huu alipotua klabuni hapo, na kumuachia Kiungo Mwenzake kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama ambaye anahusishwa kurejea Msimbazi kabla ya kufungwa kwa Dirisha Dogo la Usajili kesho Jumamosi (Januari 15).

Sakho amekua akitumia namba 17 katika jezi yake, ambapo kabla ya hajasajiliwa namba hiyo ilikua ikitumiwa na Chama ambaye aliondoka mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kusajiliwa na RS Berkane ya Morocco.

Mmoja wa viongozi wa Simba SC ambaye hakutaka jina lake litajwe hadharani amesema, baada ya Sakho kukubali kumuachia Chama namba 17, yeye atavaa namba 10 ambayo ilikua inatumiwa na Kiungo Ibrahim Ajib aliyetimkia Azam FC kufuatia mkataba wake kuvunjwa klabuni hapo.

“Chama ndio sapraizi inayosubiriwa baada ya viongozi wa Simba kumalizana na klabu yake ya Berkane FC, muda wowote kuanzia sasa atarejea nchini na tayari ameomba kuvaa jezi yake namba 17,”

“Ombi la Chama limekubaliwa baada ya Pape Ousmane Sakho kukubali kumwachia Chama jezi namba 17 huku yeye akiomba kuvaa namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Ibrahim Ajibu,” amesema kiongozi huyo

Chama anatarajiwa kutambulishwa na Uongozi wa Simba SC wakati wowote kuanzia leo Ijumaa (Januari 14), huku Dirisha Dogo la Usajili likitarajiwa kufungw arasmi kesho Jumamosi (Januari 15).

Wanne mbaroni kwa kula nyama za watu
Medo: Mtashinda huko, sio Mkwakwani