Kiungo wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Clatous Chama ‘Tripple C’ amesema kuwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakuwa na ushindani kutokana na jinsi wachezaji wapya wanaosajiliwa.

Chama ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mtandao wa Instagram akiwa live na ametoa nafasi kubwa kwa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC, kufanya vizuri kutokana na usajili wanaoendelea kuufanya mpaka sasa.

Natumaini usajili unaofanyika na Azam ni dhahiri utaleta ushindani mkubwa msimu ujao kwenye Ligi, lakini pia itakuwa poa kuona Azam ikishinda kwa ajili ya mataji na vyote unajua tusiwe tu na Ligi ya Simba na Yanga, mara hii nadhani azam FC wamesajili vizuri” alisema.

Chama alisema kuwa wachezaji wengi wanaosajiliwa na kikosi hicho anawajua na anadhani watajenga timu bora watakapokuwa na muunganiko, huku akitoa rai kuwa viongozi wanapaswa kuwa makini kwenye usajili kwani wanaweza wakasajili wachezaji wapya lakini timu ikashindwa kuwa na muunganiko mzuri.

Wanachama wamjibu Haji Manara
Kumwembe: Nina mashaka na usajili wa Makambo