Chama tawala cha Burundi CNDD-FDD, kimemteua katibu wake mkuu kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa Burundi utakaofanyika Mei 2020.

Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye ameteuliwa kama mgomba wa urais, kumrithi Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.

Jana, Jumapili  katika kikao kilichofanyika Gitega, mji mkuu wa kisiasa baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa saa tatu ya chama tawala cha CNDD-FDD, Jenerali Ndayishimiye aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho.

Ndayishimiye ni miongoni mwa wanasiasa mashuhuri katika siasa za Burundi waliokaribu na Pierre Nkurunziza.

Pia ni miongoni mwa waliokuwa waasi wa CNDD-FDD aliyejiunga baada ya kunusurika katika mauaji ya kikabila ya wanafunzi wa Wahutu katika chuo kikuu cha Burundi mwaka 1995.

Kabla ya kuteuliwa kwake, alikuwa Waziri wa mambo ya ndani na ulinzi wa umma.

Baada ya chama cha CNDD-FDD kusaini makubaliano ya Amani ya kuratibu kikosi cha taifa cha jeshi la ulinzi, Ndayishimiye alichaguliwa kama msimamizi mkuu wa jeshi na kuwa msaidizi wa jeshi wa Rais Nkurunziza.

Mwak 2018, Rais Pierre Nkurunziza alitangaza kwamba hatasimama tena katika kinyang’anyiro cha kugombea urais baada ya kubadilisha katiba ya nchi, hatua ambayo ilionekana na wengi kama njia ya wazi ya kutaka kusalia madarakani milele.

Awali wiki iliyopita, Bunge la Burundi lilipitisha sheria ya marupurupu ya kustaafu ya $530,00, jumba la kifahari na mshahara mzuri wa kila mwezi kwa kipindi kilichosalia hadi Bwana Nkurunziza atakapoondoka madarakani.

Trump, Obama wamlilia Kobe Bryant
Serikali kuendelea kuzuia mikutano ya kisiasa isiyofuata sheria