Ndoa ya mwimbaji Jose Chameleone na Daniella Atim iko kwenye wakati mgumu ambapo mwimbaji huyo ametangaza kuwa ‘bachala’.

Chameleone ametumia akaunti ya Facebook kutangaza kinachoendelea kati yake na mkewe, akieleza kuwa wamejaribu kutengeneza lakini wameshindwa.

Hata hivyo, wakati watu wengi wanaamini kuwa itakuwa ni kiki tu za mitandaoni, amewataka kuendelea kuamini wanachoamini lakini amesisitiza kuwa ni kitu halisi.

“Kila kitu kina mwisho. Nimeshindwa, sikuwa mtu bora zaidi kama ilivyonipasa kuwa! Tunahitaji nini tena? Mungu alitubariki, alitupenda, na ataendelea kuwa nasi,” tafsiri ya alichoandika Chameleone kwa lugha ya kiingereza kwenye mtandano huo.

“Watu wapumbavu watadhani ni kiki na mawazo yao ya kipumbavu. Lakini sisi tunaofahamu tunayoyapitia… inatosha!,” aliongeza.

Katika maelezo hayo marefu, mwimbaji huyo aliweka wazi kuwa hatafuti mtu wa kuchukua nafasi, “I am single and not searching!”

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa Chameleone na Daniella kupata misukosuko na kuweka wazi mitandaoni. Mashabiki wao wameendelea kuwaombea warejee katika hali salama na maelewano.

Wawili hao wamekuwa wanandoa kwa miaka 10 na kubarikiwa kupata watoto watano.

Juzi, Daniella pia aliweka kwenye Facebook ujumbe kwa watoto wake ambao unaonesha kuwa kuna tatizo katika familia hiyo.

Watoto wa kiume wa Chameleone na Daniella

Katika ujumbe huo, Daniella anawaambia watoto wake wa kiume kuwa wajenge tabia ya kuomba msamaha pale wanapokosa, kwani kwa kufanya hivyo ni kufanya tendo jema na itawapa ushindi.

“Wanangu wa kiume, Septemba ni mwezi mliozaliwa na ninataka kuwakumbusha kitu ambacho mnakijua tayari, thamani ya kile ambacho nimekuzwa nacho pia, wakati wote sema SAHAMANI ya dhati unapomkosea mtu, ni tendo la tabia njema na litakupa ushindi mara nyingi”.

Suge Knight atupwa jela miaka 28
NEC yampa Mbowe siku 7 kuomba radhi

Comments

comments