Siku chache zilizopita rapa mahiri kutoka nchini Marekani Chancelor Johnathan Bennett, maarufu Chance the rapper, alitembelea nchini Ghana akiwa na rapa mwenzake Vic Mensa.

Hii imekuwa mara yake ya kwanza kwa Chance the rapper kutembelea Ghana Ipasavyo, ambapo safari hii imekuwa ya kutimiza mengi ambayo msanii huyo hakuwahi kukutana nayo kwenye maisha yake.

Chance the rapper na wenzake siku ya jana Jumapili ya januari 9, 2022. walifanikiwa kuhudhuria katika kanisa moja huko Accra ambapo rapper huyo alifichua kuwa bibi yake mkubwa alikuwa miongoni mwa watu waliosaidia kuanzishwa kwa kanisa hilo.

“Huyu askofu Nkansah, alimfahamu bibi yangu mkubwa,” aliandika kwenye moja ya video iliyorekodiwa kanisani wakati kiongozi wa ibada akihutubia.

Katika chapisho jingine, Chance The Rapper alifichua kuwa kwa kusema kuwa babu yake mkubwa alikuwa Muafrika na nahodha chini ya mwanaharakati Marcus Garvey.

Katika kuendelea kuthibisha historia ya familia yake na nchi ya Ghana Chance rapper aliweka picha yenye kuonyesha shule na kuamdika maneno yalisimeka “Walijenga Shule hii huko james Town pia”

Licha ya kusema hayo bado haijafahamika kwa undani zaidi ni mzazi yupi kati ya wazazi wa msanii huyo mwenye asili ya nchini Ghana.

Katika hatua nyingine Sarkodie amesikia kilio cha Chance The Rapper cha kutaka kuonana naye.

Baada ya mengi ambayo ameyafanya msanii kutoka nchini Marekani Chance the rapper akiwa nchini Ghana, hatimaye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter amesema wazi kuwa amefanikiwa kufanya kila kitu nchini humo isipokuwa kukutana na msanii Sarkodie.

Punde baada ya Chance rapper kuandika ujumbe huo, hatimaye umemfikia Sarkodie ambaye naye ameonyesha kuvutiwa na kile kilichoandikwa na Chance the rapper kiasi cha kujibu kwa kusema kuwa wataonana kabla ya Chance the rapper kuondoka nchini humo.

Ujumbe wa awali aliouandika rapa huyo wa Marekani umedhihirisha kiwango cha heshima aliyonayo kwa msanii Sarkodie.

Babu wa Squid Game ashinda tuzo ya Golden Globe
Sababu za mafanikio ya Shatta Wale ni hizi...