Mwanamuziki, Chancelor Jonathan Bennett maarufu ‘Chance The Rrapper’ amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa akagombea nafasi ya meya wa jiji la Chicago baada ya kupishana mtazamo na meya wa sasa wa jiji hilo, Rahm Emmanuel ambaye amekuwa akituhumiwa kwa vitendo vya kujihusisha na rushwa,

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mwanamuziki huyo kuandika kwenye ukurasa wake wa Twetter, “Nadhani ninaweza” ambapo ujume huo ulianza kutafsiriwa kuwa huenda rapper huyo akatangaza kugombea nafasi hiyo ya uongozi msimu ujao wa uchaguzi.

Aidha, chance ameitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo anatarajia kuweka wazi tamko lake na msimamo wake juu ya ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake huo.

 

JPM afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali
Basi la New Force lapata ajali Mlima Kitonga

Comments

comments