Zao la parachichi linalozalishwa mkoani Njombe limeelezwa kukosa ubora hali inayopelekea kushindwa kuhimili katika ushindani wa soko la Kimataifa.

Hayo yamesemwa na afisa masoko wa Seasons Orchard LTD, Karim Kassam katika semina ya mtandao wa wakulima wa zao la parachichi mkoa wa Njombe, amesema zao hilo limekuwa likiwaangusha wanapofika katika soko la kimataifa ili kupamba na mazao yenye thamani.

Amesema zao hilo linatajwa kumkomboa mkulima lakini wamekuwa wakilima bila ya kuwa na elimu yoyote hali inayopelekea kulima kwa mazoea.

‘’Zao hili linatajwa kumkomboa mkulima lakini bado kunachangamoto kubwa kwa upande wa uzalishaji unaozingatia ubora….tunapopeleka katika soko la kimataifa mfano tani 300 zaidi ya tani 100 zinakataliwa….hivyo basi katika soko la nje bado tunaushindani mkubwa’’ amesema Kassam.

Aidha, Wadau wa zao hilo, Obedi Mgaya amesema changamoto ni kwamba zao hilo linakabiliwa na ugonjwa wa fangasi ambao umekuwa tishio kutokana na wakulima wa zao hilo kukosa kiuatilifu sahihi ambacho hakitashusha ubora wa tunda hilo katika masoko ya nje ya nchi.

Naye, Adrian Balongo amesema wakulima wengi nchini wamejikita katika kulima zao hilo lakini wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa elimu hasa ya magonjwa.

Kwa upande wa mratibu wa mtandao wa wakulima wa zao la Parachichi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole, amesema wakulima wanazalisha zao hilo kwa kiwango kidogo kutokana na  idara ya kilimo mkoani humo kutoingia kazini kwa ajili ya kuwasaidia wakulima kwa ajili ya kuwapa elimu sahihi juu ya ulimaji wa zao hili.

Biashara united yatambulisha kocha mpya
Video: Kitabu chenye taratibu muhimu za kufuata kujenga viwanda chazinduliwa

Comments

comments