Shirika la afya Duniani (WHO) na Serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasi ya Congo wameanzisha mpango wa kutoa chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola ili kudhibiti kusambaa zaidi kwa virusi vya ugonjwa huo.

WHO limesema kuwa limetambua zaidi ya watu 500 ambao wana dalili za kupata ugonjwa huo ambao ni tishio kubwa nchini humo.

Aidha, awamu ya kwanza ya chanjo hiyo ya majaribio iliwasili nchini Congo siku ya Jumatano ambapo tayari imeshaanza kufanyiwa kazi.

Hata hivyo, Ugonjwa wa Ebola uliua zaidi ya watu 11,000 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea, wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo mwaka 2014-2015.

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike  Hispania
Kumbukumbu ya miaka 22 tangu kuzama kwa MV Bukoba