Serikali kupitia muongozo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuanza kutoa chanjo Agosti 3 2021 mikoa yote Tanzania katika vituo 550 vya kutolea huduma

Aidha serikali imetoa angalizo kwa wasimamizi wa chanjo hospitali za umma na binafsi kutolipisha watu fedha kwani chanjo hizo ni bure huku ikihimidha kuzingatiwa kwa weledi.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi wakati wa usambazaji wa chanjo hizo kwenda mikoa mbalimbali nchini tukio lililofanyika bohari kuu ya dawa MSD, Kurasini Dar es salaam.

Amesema kuwa, Pamoja na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kufanikisha upatikanaji wa chanjo hizo na kuanza kuchanja Wananchi, Wizara ya afya inaendelea kuwashauri Wananchi kuendelea kujikinga na UVIKO-19 kwa kuzingatia unawaji mikono, kuvaa barakoa, kukaa umbali za mita moja au zaidi, kuepuka misongamano na kufanya mazoezi.

Aidha Katibu Mkuu Prof. Makubi amesema kuwa, kutokana na Mwongozo wa Chanjo wa Taifa dhidi ya Ugonjwa wa Uviko 19 Shirika la Afya Duniani WHO kwa maelekezo ya Covax Facility Chano zinatolewa kwa kufuata vipaumbele vya makundi yenye uhitaji maalum kutokana na upungufu wa uzalishaji wa chanjo toka viwandani.

Makundi ambayo yataanza chanjo ni pamoja na Watumishi wa sekta
ya Afya, Watu wazima wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea na Watu wenye magojnwa hukua kisisitiza kuwa uchanjaji kwa makundi yote nchini ni wa hiari kwa kila mwananchi.


Tanzania bingwa CECAFA U23
Afungwa miaka 20 jela kisa vipande vinne vya nyumbu