Daraja la Sigiri katika jimbo la la Budalangi nchini Kenya lililovunjika jana chache likiwa kwenye hatua za mwisho za ujenzi limezua utata nchini humo.

Daraja hilo lililogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.2 za Kenya kutoka kwenye mfuko wa Serikali, liliporomoka jana ikiwa ni siku chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake, William Ruto kulitembelea  na kuahidiwa kuwa lingekamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Ingawa sababu rasmi za kuanguka kwa daraja hilo hazijawekwa wazi, kuna utata umeibuka kuwa ujenzi wa haraka uliofanywa kwa lengo la kuhakikisha Rais anapofika akute maendeleo zaidi, huenda ni sehemu ya chanzo cha tukio hilo.

Wakati wa ziara hiyo ya rais, meneja mradi huo unaojengwa na kampuni kutoka nchini China, Jerome Xzue alimwambia rais Kenyatta kuwa hawakujikita zaidi katika barabara kwenye eneo hilo la Kaskazini bali katika daraja na kingo zake kwani ndio tatizo kubwa.

“Tunatarajia kukamilisha ujenzi wa daraja mwishoni mwa mwezi Juni kwa pande zote za Kusini na Kaskazini, kwa urefu wa kilometa 3 ili lianze kutumika mwezi Julai,” alisema Meneja Xzue.

Mbunge wa jimbo hilo, Ababu Namwamba alimshukuru Rais Kenyatta kwa ujenzi wa daraja hilo na kueleza kuwa litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo kwani wataweza kufika kirahisi sokoni, shuleni na hospitalini.

Daraja hilo limekatika ndani ya kipindi cha wiki mbili baada ya ahadi hizo, na limeanguka bila kupitiwa na kitu chochote kizito.

Mwinyi ampa tano Magufuli
Rais wa Brazil kikaangoni, aburuzwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi