Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa hawezi kutenga fedha kwa ajili ya mjadala wa mabadiliko ya Katiba mpya hivyo amewataka Watanzania wachape kazi katiba itafuata kwa wakati wake.

Ameyasema hayo jijini Dar esalaam wakati wa Kongama la hali ya uchumi na siasa nchini katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano.

Rais Magufuli amesema kuwa hategemei kutenga fedha kwa sasa kwa ajili ya kurejesha mchakato wa Katiba mpya.

“Nafahamu hamu ya watanzania kuwa na katiba mpya, sasa tunafanyaje!? Tunaendelea na hii rasimu pendekezwa au tunaenda kwenye ile ya kwanza iliyofanywa na Jaji Warioba!? Sasa badala ya kuanza kujibizana na haya ngoja tuchape kazi,”amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amebainisha kuwa anakutana na changamoto pindi anapofanya uteuzi mbalimbali hasa kwa wanawake ikiwemo madai anayopelekewa ambayo hayana ukweli na kuahidi kuendelea kuwapa nafasi kwenye uongozi wake.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wakati akifanya uteuzi wa wanawake amekuwa akituhumiwa kuteua watu ambao ana mahusiano nao mbali na mahusiano ya kikazi.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 2, 2018
Kesi ya Wema yapelekwa mbele, aachiwa huru kwa dhamana ya mamilioni