Katika hali ya Taharuki Kocha na mchezaji wa zamani wa Young Africans Cherlsea Boniface Mkwasa ‘Master’ amefikia maamuzi ya kuachana na Klabu ya Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wa 2022/23.

Mkwasa anaondoka Ruvu Shooting huku akiiacha katika hali mbaya, kutokana na matokeo mabovu yaliyopatikana siku za karibuni, huku mchezo wake wa mwisho kama Kocha Mkuu klabuni hapo alikishuhudia kikosi cha maafande hao kilikubali kupigwa 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC mjini Singida katika Uwanja wa Liti.

Hata hivyo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa Ruvu Shooting Masau Bwire amezungumza na Dar24 Media na kueleza kuwa, Mkwasa ameomba kuondoka klabuni hapo, ili kutoa nafasi kwa Kocha mwingine ambaye huenda kawa na bahati ya kuiweka mahala salama klabu hiyo yenye maskani yake Mlandizi mkoani Pwani.

Masau Bwire amesema licha ya jitihada zilizotumiwa na Uongozi wa Ruvu Shooting kumshawishi Kocha huyo abaki, bado uamuzi wake wa kutaka kuondoka ulibaki kama alivyoupanga, hivyo wakaona ni bora waheshimu alichokiamua.

“Ametaka kuondoka yeye kama Kocha, alichokifinya ameuandikia Uongozi barua ya kutaka ajiuzulu nafasi yake, japo Uongozi haukukubaliana naye, tulikaa naye chini ili kumshawishi asiondoke lakini alibaki na uamuazi wake.”

“Kubwa alilolitaka yeye ni kutoa nafasi kwa kocha mwingine kwa kuamini huenda akawa na Bahati ya kuiweka mahala salama Ruvu Shooting, ambayo kwa sasa ninakiri hatufanyi vizuri katika Michezo ya Ligi Kuu.”

“Licha ya kumkubalia kuondoka bado tutaendelea kumtumia Mkwasa kama sehemu ya ushauri katika upande wa kiufundi kwa sababu tumefanya naye kazi kwa kipindi kirefu na anaijua klabu yetu ipasavyo, Tunamtakia kila la Kheir.” amesema Masau Bwire

Hadi sasa Ruvu Shooting imeshashuka Dimbani katika michezo 15 ya Ligi Kuu Tanzaia Bara, ikishinda mitatu, ikitoka sare miwili na kupoteza 10.

Kwa matokeo hayo Ruvu Shooting inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Papic: Kwa nini Simba SC, Young Africans haziamini wazawa?
Mwanachama Simba SC walitwa kuchukuwa FOMU