Klabu za jijini London nchini England, Chelsea na Arsenal zimeanza kuonyesha makeke ya kuihitaji saini ya kiungo wa mabingwa wa soka wa EPL, Leicestter City, N’golo Kante.

Chelsea na Arsenal zimekua za kwanza kuonyesha makeke ya kumuwania kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, kutokana na hamasa ambazo zimeanza kuchukua nafasi ndani kwa ndani kwenye makao makuu ya klabu hizo.

Ushujaa na kujituma kwa Kante katika kipindi chote cha msimu wa 2015-16, kumekua chagizo la klabu hizo mbili kufikiria namna ya kumsajili mara baada ya dirisha litakapofunguliwa siku kadhaa zijazo.

Hata hivyo tayari kuiungo huyo kutoka nchini Ufaransa, ameshatahadharishwa na meneja wa Leicestter City, Claudio Ranieri juu ya kutokufanya maamuzi ya kusaka mahala pengine pa kucheza msimu ujao na badala yake afikirie kubaki King Power Stadium.

Mbali na klabu hizo za jijini London, pia mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint Germain (PSG) nao wamejitangaza hadharani kumuwania Kante huku wakiamini kiasi cha Pauni million 19.7 kitatocha kuvunja mkataba wake.

Kante ambaye anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa ambacho kitashiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016) mwezi ujao, amekua akilipwa mshahara wa Pauni elfu 25 (25,000) kwa juma tangu alipojiunga na Leicester City mwanzoni mwa msimu huu.

Udhaifu huo wa malipo umebainiwa na viongozi wa klabu hiyo na sasa wanajipanga kumuandalia mkataba mpya ambao utamuwezesha kulipwa vizuri.

Kigezo cha mshahara wake kimekua kikitajwa kama sehemu ya kuzishawishi klabu nyingine kumuwania kwa urahisi Kante katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu.

Serikali 'Yamfungia' Snura Na Chura Wake!
Cristiano Ronaldo yupo Fit Kwa Asilimia 100