Chama cha soka nchini England FA, kimeziadhibu klabu za Chelsea na Arsenal kufuatia zogo lililoibuka baina ya wachezaji wa pande hizo mbili, wakati wa mchezo wa ligi ya nchini humo uliochezwa Septemba 19 kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Klabu hizo zimetozwa faini, baada ya kubainika kulikua na uzembe kwa viongozi wa mabenchi ya ufundi, kwa kushindwa kuwatuliza wachezaji wao ambao walionekana kuwa na jazba kufuatia tukio lililojitokeza baina ya Diego Costa dhidi ya Gabriel Paulista.

Chelsea na Arsenal wamatozwa faini ya paund 40,000 na 30,000 sambamba na kupewa onyo kali kwa kutakia kutorejea kosa kama hilo kwenye michezo iliyo chini ya chama cha soka nchini England.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, FA waliziamuru klabu hizo kuwasilisha utetezi wa matukio ya utovu wa nidhamu kwa wachezaji yaliyoonekana katika mchezo huo, na imebainika pande zote mbili zilishindwa kutumia busara ya kukabilina na makosa yaliyojitokeza.

Mchezo huo uliomalizika kwa Arsenal kufungwa mabao mawili kwa sifuri, ulishuhudia beki Gabriel Paulista akionyeshwa kadi nyekundu kutokana na kitendo cha kutaka kumpiga teke kwa nyuma Diego Costa, lakini baadae FA waliifuta adhabu hiyo kufuatia rufaa iliyowasilishwa na Arsenal kupinga maamuzi yaliyochukuliwa na muamuzi Mike Dean.

FA, pia walimchukulia hatua za kinidhamu mshambuliaji Diego Costa, baada ya kupitia taarifa za muamuzi na kurejea picha za televisheni ambapo ilibainika alimpiga kibao na kumsukuma kwa makusudi beki wa Arsenal, Laurent Koscielny katika dakika ya 44.

Costa alifungiwa kucheza michezo mitatu inayosimamiwa na chama cha soka nchini England.

Kinana Hamuachii Lowassa, Hakumbuki Chochote…
Utata Vifaa Vya ‘BVR’ Vilivyokamatwa Vikiandikisha Wafanyakazi Dar