Klabu ya Chelsea inajipanga kumrejesha mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Romelu Lukaku ambaye aliuzwa klabuni hapo chini ya utawala wa Jose Mourinho mwaka 2014, na kusajiliwa na klabu ya Everton.

Lukaku amekua akishinikiza kuondoka Goodson Park, kwa lengo la kuhitaji mahala pengine pa kucheza soka lake, hatua ambayo imewaaminisha Chelsea wanaweza kumrejesha kwa urahisi chini ya utawala wa meneja wao wa sasa Antonio Conte.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amekua na mazingira mazuri ya kucheza soka lake kwa uhuru tangu aliposajiliwa na Everton kwa mkopo mwaka 2013, kabla ya kusajili moja kwa moja mwishoni mwa msimu wa 2013-14.

Hata hivyo Chelsea huenda wakapata upinzani katika harakati za kumrejesha mshambuliaji huyo Stamford Bridge, kutokana na jina la Lukaku kuwa sehemu ya wachezaji wanaopigiwa chepuo la kujiunga la Man Utd.

Klabu nyingine zinazotajwa kuwa katika mpango wa kumuwania mshambuliaji huyo ni Paris Saint-Germain (Ufaransa), Bayern Munich (Ujerumani) pamoja na Real Madrid (Hispania).

Lukaku, aliondoka Chelsea na kujiunga na Everton kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 28, na kwa sasa amewekwa sokoni kwa thamani ya Pauni milioni 65.

Gabriel Omar Batistuta Amkingia Kifua Francesco Totti
Mourinho Adhamiria Kuwafundisha Adabu Chelsea