Klabu ya Chelsea usiku wa kumakia hii leo ilishindwa kufurukuta mbele ya Watford katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana.

Chelsea ambao walikua wakipewa nafasi kubwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo kufuatia matokeo ya michezo yao miwiwli iliyopita dhidi ya Arsenal pamoja na Milton Keynes Dons kuwa mazuri.

‘Attack, attack, attack,’ ulikuwa wimbo kutoka kwa mashabiki wa Chelsea wakimaanisha wanachotaka wao ni soka la kushambulia.

Meneja wa muda wa klabu hiyo magharibi mwa London, Guus Hiddink anafanikiwa kuendelea kudumisha rekodi yake ya kutofungwa tangu achukue mikoba ya Jose Mourinho, lakini bado ana kazi nzito ya kutengeneza timu ya ushindi.

Costa was booked for his part in the confrontation as Chelsea were frustrated at Vicarage Road by a spirited Watford side

Mshambuliaji tegemeo wa Chelsea Diego Costa alishindwa kung’ara na kuhusika kwenye matukio saba ya ukorofi hali iliyomfanya aambulie kadi ya njano.

Watford (4-3-2-1): Gomes 7.5; Paredes 6.5 (Nyom 67, 6), Prodl 7, Cathcart 7, Holebas 6.5; Capoue 6.5 (Suarez 86, 6), Watson 6.5, Behrami 6; Jurado 7 (Abdi 63, 6); Deeney (c) 7, Ighalo 7

Chelsea (4-2-3-1): Courtois 7; Ivanovic 6, Zouma 6.5, Terry (c) 6, Azpilicueta 6; Mikel 6, Matic 7 (Hazard 72, 6); Willian 7, Fabregas 6, Oscar 7; Diego Costa 6.5

 

Wabaguzi Wasababisha Game Ya SS Lazio Vs SSC Napoli Kuahirishwa
FC Barcelona Yamuaibisha Gary Neville Hispania