Kikosi cha Chelsea kimelazimika kumaliza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Liverpool, kikiwa pungufu baada ya kiungo kutoka nchini Hispania, Cesc Fabregas kuonyeshwa kadi nyekundu.

Chelsea walipambana na Liverpool katika mchezo wa michuano ya International Champions Cup (ICC), inayoendelea nchini Marekani kwa lengo la kuziandaa baadhi ya klabu za barani Ulaya kwa ajili ya msimu wa 2016/07 ambao utaanza rasmi mwezi ujao.

Fabregas, alionyeshwa kadi nyekundu, baada ya kumchezea ndivyo sivyo beki wa Liverpool, Ragnar Klaven.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp ameonyesha kuchukizwa na mchezo wa hovyo ulioonyeshwa na Fabregas, ambao umepelekea kumumia kwa Klaven.

Katika mchezo huo Chelsea wamechomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na beki kutoka nchini England, Gary Cahill katika dakika ya 10.

Saa 48 Zijazo Kuamua Hatma Ya Paul Pogba
Video: ‘Conveniently rolling‘ ya Koku Gonza