Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal) wamewasilisha maombi kwenye klabu za Valencia na West Brom, wakitaka kuwasajili Shkodran Mustafi na Jonny Evans.

Arsenal wamewasilisha maombi hayo, lakini hawajaweka mezani dau kwa wachezaji hao wawili.

Huenda The Gunners wakapata upinzani mkali kutoka kwa Chelsea ambao wameonyesha nia ya kumsajili Mustafi, ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Everton.

Mkataba wa beki huyo kutoka nchini Ujerumani, unaonesha kuwa, kama kuna klabu itataka kumsajili inatakiwa kutoa kiasi cha Pauni milioni 41, lakini Valencia wamejishusha na kuwa tayari kupokea hadi Pauni milioni 25.

Jonny Evans

Arsenal wanahitaji kuongeza beki mpya, baada ya nahodha wao Per Mertesacker kusumbuliwa na majeraha ambayo huenda yakamuweka nje hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Beki huyo wa Ujerumani alipata majeraha hayo wakati wa mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya RC Lens, ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Video: MOI yakanusha taarifa iliyotolewa na gazeti la Mwananchi
Manny Pacquiao kurejea ulingoni Novemba 5 na bondia huyu