Meneja mpya wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte ameanza kushughulika na mpango wa kutaka kumng’oa mshambuliaji wa klabu bingwa nchini Italia Juventus, Álvaro Borja Morata Martín.

Conte ameanza mpango huo, kwa kuamini kwake itakua rahisi kumpata Morata, kutokana na ukaribu uliopo baina yao, hasa ikizingatiwa alimsajili kwa mkopo akitokea Real Madrid miaka minne iliyopita.

Hata hivyo, kuna hatari ya kuibuka kwa ushindani wa usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, kutokana na taarifa kueleza kwamba, baadhi ya klabu za barani Ulaya ikiwepo Real Madrid zinajipanga kumsajili.

Madrid wamedhamiria kumrejesha Morata, kwa lengo la kuongeza chachu ya ushindani kwenye safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inaongoza na Cristiano Ronaldo, Karim Banzema pamoja na Gareth Bale (BBC).

Licha ya matarajio hayo, gazeti la michezo la nchini Italia liitwalo Gazzetta dello Sport, leo limetoka na habari inayoeleza kwamba, Antonio Conte ameuagiza uongozi wa Chelsea, kutuma ofa ili kuanza mipango ya kumsajili mshambuliaji huyo.

Klabu zingine ambazo zinatajwa kuwa kwenye mipango ya kumsajili Morata, ni Arsenal pamoja na Man City.

Silvio Berlusconi Kukutana Na Wafanyabiashara Wa China
Viongozi Wa Arsenal Wamfikiria Upya Arsene Wenger

Comments

comments