Mabingwa wa soka nchini England (Chelsea), wameongeza sura mpya kikosini kwao baada ya hii leo kumsajili aliyekua mlinda mlango wa Manchester City, Willy Caballero.

Caballero mwenye umri wa miaka 35 amejiunga na Chelsea kwa uhamisho huru baada ya kuachwa na Manchester City mwishoni mwa msimu uliopita.

Chelsea imeamua kumsajili Caballero anayetokea Argentina ili kuchukua nafasi ya aliyekuwa kipa wake chaguo la pili, Asmir Begovic aliyejiunga na Bournemouth kwa dau la Pauni milioni 8.

Caballero anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Chelsea katika siku hii ya leo. Mwingine ni kinda Ethan Ampadu mwenye umri wa miaka 18, aliyetokea Exeter.

Ufaransa yatoa msaada wa Euro 250,000 kwa wakimbizi
Sandro Ramirez Atua Goodison Park