Klabu ya Chelsea imejitutumua katika harakati za kutaka kumsajili beki kutoka nchini Cameroon na klabu ya SSC Napoli, Kalidou Koulibaly kwa kuwasilisha ofa ya Pauni milioni 48.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa Chelsea wanaamini ofa hiyo itatosha kufakisha azma ya kuipata saini ya beki huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye ameonyesha kuwa katika mipango ya meneja Antonio Conte.

Usajili wa Koulibaly unapigiwa chepuo na meneja huyo kutoka nchini Italia, kwa lengo la kutaka kuziba nafasi ya beki kutoka nchini Ufaransa Kurt Zouma ambaye anaendelea kuuguza jeraha la goti alilolipta msimu uliopita.

Awali Chelsea waliwasilisha ofa ya Pauni milioni 42 kwa ajili ya kuwashawishi viongozi wa SSC Napoli, lakini hawakufanikiwa kwa kigezo cha ofa hiyo kutokuwa na thamani ya mchezaji wanaemkusudia.

Hata hivyo kuna taarifa zinadai kuwa, uongozi wa SSC Napoli utakubali kumuachia Koulibaly, endapo watapata uhakika wa kumsajili beki kutoka nchini Serbia na klabu ya Torino Nikola Maksimovic.

Mourinho Aibuka Na Bishara Ya Kubadilishana Wachezaji
Cesc Fabregas Awachunia Mashabiki Wake