Klabu ya Chelsea ipo katika mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Morocco na klabu ya Ajax ya Uholanzi Hakim Ziyech, ambaye thamani yake ni Pauni milioni 38.

Chelsea wameanza mazungumzo ya usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, wakilenga kumpeleka jijini London mwishoni mwa msimu huu, baada ya mpango wa kufanya hivyo mwezi Januari kupitia dirisha dogo kushindikana.

Uongozi wa Ajax ulishindwa kuridhia dili la kumuuza Ziyech mwezi Januari, kwa kusudio la kuhitaji huduma yake, ili kufanikisha lengo la kutwaa ubingwa wa ligi ya Uholanzi (Eredevisie) msimu huu.

Endapo mambo yatakwenda kama yalivyopangwa, usajili wa Ziyech utakua wa kwanza kwa meneja wa sasa wa Chelsea Fank Lampard, ambaye alianza majukumu yake klabuni hapo, kwa kukuta adhabu ya kufungiwa kusajili iliyotolewa na shirikisho la soka duniani FIFA.

Mbali na Ziyech, Chelsea ilihusishwa na mpango wa kusajili wachezaji kadhaa wakati wa dirisha dogo (Mwezi Januari) akiwepo mshambuliaji wa mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain Edinson Cavani na Dries Mertens wa SSC Napoli ya Italia.

Kocha wa Misri asubiri maamuzi ya Mohamed Salah
Tanzia: Aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda afariki dunia

Comments

comments