Baada ya kumkosa Romelu Lukaku aliyetimkia Man Utd Klabu ya Chelsea inataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero.

Chelsea wamekuwa wakihusishwa na kutaka kuwasajili washambuliaji tofauti akiwemo Alvaro Morata kutoka Real Madrid, Pierre-Emerick Aubameyang  wa Borussia Dortmund, Andrea Belotti kutoka Torino na sasa Sergio Aguero.

Tangu imenunuliwa na  ‘Abu Dhabi United Group’ klabu ya Manchester City haijawahi kumuuza mchezaji ambaye bado inamuhitaji.

Alipoulizwa kama Aguero atabaki Man City mwenyekiti wa klabu hiyo Khaldoon Al Mubarak alisema mchezaji huyo bado ni mmoja wa kikosi cha City na ni lazima abaki katika timu hiyo.

”Aguero ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani na sisi ni timu inayotaka kushinda mashindano yote” aliongeza mwenye kiti wa Man City Khaldoon Al Mubarak.

Baada ya Aguero kuwa mfungaji bora wa Man City msimu uliopita kwa kufunga mabao 20 na kufunga mabao mawili katka mchezo wa mwisho wa 5-0 dhidi ya Watford Pep Guardiola alisistiza kuwa mchezaji huyohauzwi.

”Kila mahojiano na waandishi wa habari mnaniuliza wsali hili haya sasa Aguero atakuwa na furaha vizuri msimu ujao” alisema Guardiola.

Mchezaji huyo alisajiliwa na Man City mwaka 2011 kutoka Atletico Madrid kwa kiasi cha Pauni milioni 38 na ameifungia Man City mabao 169 mpaka sasa huku akishinda makombe mawili ya ligi kuu ya Uingereza.

 

AC Milan Yajitosa Kwa Alvaro Morata
Sterling: Sina Shaka Na Ubingwa Wa PL

Comments

comments