Chid Benz ameonesha kuchukizwa na maoni ya Afande Sele kuhusu mwenendo wake wa maisha baada ya Mfalme huyo wa Rhymes kudai kuwa hawezi kupandishwa kwenye jukwaa la Tamasha la Wasafi.

Katika video hiyo ya mashambulizi kwa Chid Benz aliyoiweka Instagram, Afande anafunguka akieleza kuwa tabia ya uteja wa dawa za kulevya haina tofauti na tabia ya ushoga, neno ambalo linaonekana kumkasirisha Chid ambaye ameendelea kusisitiza kuwa ameacha kutumia dawa hizo.

Rapa huyo kutoka Ilala amemtumia ujumbe Afande Sele kupitia mahojiano aliyofanya leo na vyombo vya habari, akieleza kuwa kwanza hakuwahi kumtaja katika maelezo yake yoyote hivyo anamuona kama ameingilia kisichomhusu.

Mkali huyo wa ‘Dar es Salaam Stand Up’, amemtaka Afande Sele ambaye anashikilia taji la Mfalme wa Rhymes, afahamu kuwa pindi watakapokutana itakuwa ni muda wa kuzungumza wao wawii ili wayamalize.

“Ukiacha matukio ya nyuma, tunaanza leo. Tutakapokutana na wewe na iwe ni mimi na wewe. Mama yangu haingilii, baba yangu haingilii, sijui kuhusu wewe lakini ni mimi na wewe, personal. Wale ambao wana issue niliyozungumzia ni wale. Hii ninaongea na wananchi wanajua kuwa Chid huwa anakwenda hivyo na huwa anamaliza kesi hivyo,” Chid amefunguka.

Katika hatua nyingine, Rapa huyo amewaomba radhi mashabiki kwa majibizano yanayoendelea kufuatia kauli zake, na ametumia nafasi hiyo kutangaza kuwa ataachia wimbo wake mpya muda wowote kwa ajili ya mashabiki wake.

Sirro afanya mabadiliko madogo ndani ya jeshi la polisi
Vichanga 10 wanusurika kukeketwa

Comments

comments