Katibu Mkuu wa Chama Cha Wamiliki wa Sober House Tanzania, Pilli Missanah ameomba jamii isimnyanyapae wala kumnyoshea vidole msanii wa muziki wa Bongo Fleva Chid Benz ambaye tayari ameathirika kwa kutumia dawa za kulevya na mara kadhaa amekuwa akishikwa na dawa hizo.

Missanah ameamua kumfuatilia msanii huyo ili aweze kumsaidia, na amesema kusaidiwa kwake ni kumchukua na kumepeleka Sober House ili aweze kupata tiba kwani anaamini kuna uwezekano mkubwa wa msanii Chid Benz kuacha kabisa matumizi ya dawa za kulevya.

Aidha ametangaza rasmi kumtafuta Chid Benz kwa lengo la kutaka kumsaidia kutoka katika janga la utumiaji wa dawa za kulevya ili aweze kurudi katika maisha yake ya kawaida kama alivyokuwa awali.

”Mimi mpaka sasa hivi nimeshamuwekea ‘deffender’ mtaani yani akionekana tu akamatwe hata kwa nguvu ili wamlete kwangu”.

“Mimi ndio mtu wa kwanza kumshauri Chid Benz aje Sober house, nimeshamfuatilia sana na hata sasa hivi bado naendelea kumfuatilia ili niweze kumsaidia kwasababu ni kijana bado tuna muhitaji. Kuna uwezekano mkubwa wa Chid kuacha vitu anavyo vitumia na kuwa mtu wa kawaida. Ila tatizo ni moja tu anapaswa akubali tatizo na wala asifiche fiche mambo”, amesema Pilli.

“Chid anahitaji huruma yetu sisi wala tusimnyanyapae, tusimseme vibaya wala kumnyoshea vidole. Kusaidiwa kwake ni kumchukua na kumpeleka kwenye tiba ndio msaada mkubwa anaohitaji kwa sasa”. Amesema Pili Missanah.

Hayo yamezungumzwa leo kupitia kipindi cha eNews kinachoruka katika chaneli ya EATV.

Hii ndio sababu ya Ndugai kumtimua mbunge wa CUF bungeni
Rais Mnangangwa awasili Tanzania