Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na mzigo wa bangi kiasi cha gramu 5.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hayo leo Jumatatu, Juni 18, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo baada ya kumtia mbaroni msanii huyo.

Hii ni mara ya nne kwa Chidi Benz kukamatwa na madawa ya kulevya huku akidai kuwa alishaacha kutumia madawa hayo na anaendelea na matibabu Sober House.

Mnamo Disemba 30, 2017 nguli huyo wa Hip Hop Chid Benz alishikiliwa tena  na jeshi la polisi mkoani Dodoma akiwa na mke wake ambapo alikamatwa na dawa za kulevya aina ya Heroine na kufikishwa mahabusu.

Kanisa lawabatiza kwa kutumia Pombe
Hispania yakubali kuwapokea wahamiaji kutoka Afrika